SHIRIKA
Shauri ya kushirikiana lilianza kutokea na safari yetu mara ya kwanza ncini ya Kenya mnamo 1991, tulipata uwezo wa kutembelea barani Africa katika miseni na mapadri ya Consolata Torino kwamba waliofanya kazi zao shambani la Mungu palee Kenya.
Kati ya mahali tuliosafiri Kenya tunakumbuka Makuyu, Karaba Wango, Kahawa, Mombasa, Sagana, Lodokejek; Iringa pale (Tanzania), Ibadan (Nigeria), Parakou (Benin).
Kazi muhimu tuliotendeza katika miaka hiyo ni:
- Kazi ya mfuachuma na mafundisho na wasichana kwa fundi ya chuma na kujengea mikokoteni, Kitanda kwa hospitali, michezo ya watoto, baiskeli kwa walemavu, na k. wa k.
- Kuhelimisha watoto kucheza michezo pamoja kama oratori namna yake mtakatifu Don Bosco.
- Kusoma lugha tamu ya kiswahili na utamaduni ya Kenya
- Mkuu ya shirika alitengeneza kitabu kuhusu utamaduni, desturi, mila na elimu katika wakaaji wasamburu; kwa mitiani yake chuo University Torino.
Maarifa tuliopata tukifanya matendo hayo yote yatufahamisha mambo mengi na shida ya maishani yao wenyeji, mfano: shida ya ujamii, biashara, elimu na utamaduni. Tulisaidiana pia watu wakuu wanaotenda matendo maalum juu ya maendeleo ya ujamaa.
Baadaye, tarehe 7-4-2013 tulishauriana na kuanzishi shirika linaitwa “ SHAMBA” kulima matumaini.
Katika miaka iliyofuata wanachama wote walisafiri Kenya, Tanzania, Benin na Nigeria wakaishi nao mudha kwa mudha, wakifanya kasi bure kwenye aina mbali mbali, elimu pia na kusaidia wakenya na mahitaji yao.
Shirika linafuata makusudio haya:
- kushauriana na watu wa ulimwengu kuhusu matendo ya huruma na kusaidiana
- Kufahamishana juu ya utamaduni mbalimbali
- Kusaidia wahitaji wapate kazi, elimu na kuzidisha hali nzuri ya maisha katika Kenya na taifa nyingine
- Kuchuma fedha
- Mafundisho kwa ufundi
- Kutilia kazi
- Kusaidia bwanakazi kuwapatie kazi na mwenyeji
- Kusaidia elimu na afia
- Kusaidia wanawake, watoto wachanga na walemavu
Twandikie kwa kufahamishana juu ya mambo mengi. Asante sana!